Jumatatu 28 Aprili 2025 - 19:59
Kwa Nini Inatupasa Kufuata dini Maalumu?/ Je, Bila ya dini haiwezekani Mtu kuwa mwema?

Katika mfumo wa maisha, mwanadamu siku zote hutafuta nuru itakayomwonyesha njia sahihi na kumtenganisha na upotovu. Lakini je, nuru hii hupatikana tu katika taa ya dini? Au yawezekana kufikia ukamilifu kwa kushikamana na maadili pekee? Ikiwa dini ni ya lazima, basi mtu anawezaje, kutokana na wingi wa dini na madhehebu yaliyopo, kutambua njia iliyo sahihi? Majibu ya maswali haya yanatolewa katika mazungumzo haya.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, katika dunia ya leo, maswali na changamoto kuhusu dini na imani za kidini yamekuwa yakitolewa kwa wingi kuliko wakati wowote uliopita.

Miongoni mwa maswali haya muhimu ni hili lisemalo: kwa nini mwanadamu anatakiwa kufuata dini maalumu? Je, haiwezekani kuishi maisha ya kimaadili na kufikia ukamilifu bila kuwa na dini?

Ili kupata majibu sahihi na ya kimantiki kwa maswali haya, tumefanya mazungumzo na Hujjatul-Islam Reza Parchabaf, mtaalamu wa changamoto za kidini na kimaadili, na tunakukaribisha kupitia makala hii upate uelewa wa kina zaidi juu ya umuhimu wa kufuata dini na nafasi yake katika maisha ya mwanadamu.

Swali: Umuhimu wa kufuata dini ni upi? Kwa nini mtu anatakiwa kufuata dini maalumu? Je, si inawezekana kuishi maisha ya maadili mema na kufikia ukamilifu bila dini?

1. Asili na Mahitaji ya Ndani ya Mwanadamu

Mwanadamu kwa asili huuliza maswali ya msingi kama: lengo la maisha ni lipi? Ukweli wa kuwepo ni upi? Asili ya uhai ni ipi?
Dini za mbinguni, kwa kutoa mtazamo mpana duniani, hujibu mahitaji haya ya kiasili.

Qur'ani Tukufu inasema:  
"Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini - ndilo umbile la Mwenyezi Mungu alilo waumbia watu."
(Surat Ar-Rum: 30)

2. Kupenda Ukamilifu na Uongofu wa Kiungu

Ukamilifu wa kweli hupatikana tu kupitia maarifa sahihi kuhusu mwanadamu, dunia, na Mwenyezi Mungu. Dini, kama mwongozo wa kiungu, huelekeza njia ya kufikia ukamilifu huu. Bila dini, viwango vya maadili na hamu ya kufikia ukamilifu hugeuka kuwa vitu vya vinavyo badilika na visivyo thabiti.

Imamu Ali (a.s) anasema:


الدِّینُ یُصْلِحُ الْأُمُورَ الَّتِی لَا یُصْلِحُهَا الْعَقْلُ

"Dini husahihisha mambo ambayo akili haiwezi kuyasahihisha."

3. Changamoto za kufikia ukamilifu kwa kutegemea maadili pasi na dini

- Maadili ni jambo la mwelekeo wa mtu binafsi; bila ya dini, hakuna kipimo thabiti cha kutofautisha jema na ovu, bali maadili hupunguzwa hadi mitazamo ya mtu binafsi au jamii.
  
- Dini, kutokana na kutegemea thawabu za akhera na radhi za Mwenyezi Mungu, huleta motisha ya kina na ya kudumu kwenye kushikamana na maadili.

- Maadili ya kisekular kwa kawaida huzuia mafungamanobkwa wanadamu, ilhali dini huweka mfumo wa mafungamano kati ya mwanadamu na Mwenyezi Mungu, kwake yeye mwenyewe, na pia mpangilio wote wa dunia.

4. Kwa Nini Inapaswa Kufuatwa Dini Maalumu?

Iwapo tukikubali kuwa dini ni ya lazima, basi tunapaswa kutafuta dini ambayo:

- Ina asili ya kimungu (siyo ya kutungwa na mwanadamu).
- Ina upeo mpana na wa kimataifa.
- Inaoana na akili na asili ya mwanadamu.
- Inadai kuwa dini ya mwisho (kama vile Uislamu unavyodai kuwa dini kamili na ya mwisho).

Hitimisho:
Ingawa huenda mtu akazingatia baadhi ya maadili bila kuwa na dini, lakini maadili bila msingi wa kidini kuthibiti kwake ni kudogo sana.

Dini ni taa ya akili na pia ni ukamilifu wake; na bila dini, mwanadamu hupotoka katika njia ya kuelekea kwenye ukamilifu.

Mazungumzo kutoka kwa: Samira Golkar

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha